Tuesday, 5 March 2019

Lazaro Nyalandu: Sikuletwa CHADEMA na MAFURIKO


Siku chache baada ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kurudi CCM akitokea Chadema, Mbunge wa zamani wa Singida Kaskazini ambaye kwa sasa ni kada wa Chadema, Lazaro Nyalandu amesema hakuletwa kwenye chama hicho na mafuriko.


Lowassa aliyerejea CCM wiki iliyopita alijiunga na Chadema Julai 28, 2015 na kupitishwa kugombea urais kupitia chama hicho akiwakilisha pia vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) akiwa na kundi kubwa la wana CCM waliohama naye wakifahamika kama mafuriko.

Hata hivyo, Nyalandu aliyejitoa CCM Oktoba 30, 2017 na baadaye kujiunga na Chadema jana alitumia akaunti yake ya Twitter kuandika ujumbe unaoelezea  hatima yake ndani ya Chadema.

“Naamini katika kushiriki kuleta mabadiliko ya kweli Tanzania kupitia upinzani. Tusikate tamaa. Kesho ni nzuri kuliko jana,” alisema Nyalandu katika ujumbe huo.

No comments:

Post a Comment