Friday, 8 March 2019

KAULI YA KATIBU WA CCM MKOA WA MOROGORO ALIPOTEMBELEA MAONYESHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 8 MARCH 2019 UWANJA WA JAMHURI MOROGORO

 Shaka Hamdu Shaka Katibu CCM Morogoro kushoto akitazama bidhaa za wanawake wajasiriamali
Taifa lolote lisilothamini mchango wa wanawake ni  butu, dhana ya usawa wa kijinsia ni  kichocheo  cha ushiriki na ushirikishwaji katika maendeleo endelevu ya kila Taifa linalothimini na kujali mchango wa kina mama.

Baba wa Familia ya watanzania  Rais John Pombe Joseph Magufuli alisema asubuhi ya leo 8 Machi 2019 kuwa  serikali anayoiyongoza inathamini kazi nzuri inayofanywa na akina mama, amewataka muendelee kutembea kifua mbele. 

Nasi wasaidizi wake katika Chama cha Mapinduzi  tunamuunga mkono kwenye hilo ninawahakikishia tutawapa kila aina ushirikiano, msaada na tutawashika mkono wanawake wa Morogoro na watanzania kwa ujumla  ili muweze kufikia ndoto zenu  maana hata ilani ya CCM  2015-2020 imetuelekeza kusimamia na kuendeleza harakati za maendeleo ya wanawake  kiuchumi, kijamii na kiasiaza nchini.

Shaka Hamdu Shaka
Katibu CCM Morogoro

No comments:

Post a Comment