Monday, 18 March 2019

Hao ni mizigo, wachukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria - Waziri Mkuu


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaagiza viongozi wa serikali kuwawezesha Maafisa Habari kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na kwa wakati,

Waziri Mkuu amebainisha hayo leo wakati wa kikao kazi cha maafisa mawasiliano wa serikali mkoani Mwanza ambapo amewataka maafisa hao kuhakikisheni wanatekeleza majukumu yao ipasavyo.

“Serikali inathamini sana kada ya Habari, nyie ni watu muhimu sana Serikalini, epukeni Uchochezi, vijembe na kupandikiza chuki kwa jamii," amesema Waziri Mkuu.

Pia Waziri Mkuu ameonya kuwa, 'Maafisa Habari ambao hawatekelezi majukumu yao hao ni mizigo, wachukuliwe hatua kwa mujibu wa Sheria. Naiagiza Wizara ya Habari kufanya tathimini za mara kwa mara kwa Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini'.

No comments:

Post a Comment