NA MWANDISHI WETU, SONGEA
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO,  Dkt. Alexander Kyaruzi  akiaambatana na Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika  hilo wamefanya ziara katika Mikoa ya Iringa Njombe pamoja na Ruvuma ili kujionea maendeleo ya Miradi inayotekelezwa na Shirika katika Mikoa hiyo.
Katika ziara hiyo Bodi ilitembelea vituo vya Gridi vya Makambako pamoja na Madaba ambavyo vimejengwa kupitia Mradi wa ujenzi wa njia ya usafirishaji umeme wa Kilovolti 220 wa Makambako -Songea. Pia Wajumbe walipata wasaa wa kutembelea eneo la Kisada ambapo TANESCO inatarajia kujenga kituo kikubwa kabisa cha Kupoza na kusafirisha umeme chenye uwezo wa kupokea umeme utakao safirishwa katika njia ya umeme wa Kilovolti 400 ya Iringa hadi mbeya    Njia ya usafirishaji umeme itakayo ziunganisha nchi za Tanzania na Zambia. Hii ni miongoni mwa jitihada zinazo fanywa na Serikali kupitia  TANESCO   za kuunga njia za usafirishaji umeme za kusini mwa Bara la Afrika (South African power pool)
Akizungumzia umuhimu wa Miradi hii Dkt Kyaruzi alisema , inakusudia kuiunganisha nchi na mataifa mengine yanayotuzunguka kwa upande wa Kaskazini ambako kuna mradi ujulikanao kama Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK na tayari umeanza kutekelezwa (East African Power pool) pamoja na upande wa kusini katika( South African Power Pool) hii itawezesha Tanzania kuweza kunufaika na umeme unaopatikana nchi za Kenya na Ethiopia  ambao tayari watakuwa wamejiunga na mifumo yetu , vivyo hivyo kwa upande wa Zambia ambao pia tutajiunga nao.
Pamoja na kutembelea vituo hivyo wajumbe wa bodi walitembelea Kituo cha zamani cha Kufua  umeme kwa kutumia mafuta ya Dizeli cha   Songea  ambacho kimesitisha  kutumika tangu mwezi Septemba mwaka 2018 ili kupisha ujio wa umeme wa Gridi ya Taifa kupitia Mradi wa  njia ya Kusafirishaa umeme ya Kilovolti 220   ya Makambako Songea. Ambapo kuzimwa kwa kituo hicho kumeiwezesha TANESCO  kuokoa zaidi ya shilingi Milioni 430 kwa  mwezi.
 MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO,  Dkt. Alexander Kyaruzi, (wapili kushoto-mbele), na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakitembezwa kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Songea, wakati bodi ilipotembelea miundombinu ya umeme 

Mwendesha mitambo "system operator " kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Songea, Bw. Athanas James Saga akitoa maelekezo ya usalama mbele ya wajumbe wa bodi walipotembelea kituo hicho.

Picha ya Pamoja ya Wajumbe wa Bodi ya wakurugenzi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Christina Mndeme(mstari wa mbele katikati) nje ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Share To:

Post A Comment: