Viongozi wa chama cha Mapinduzi CCM wa Kata ya Kipunguni Wilayani Ilala wakiimba wimbo wa Chama Dar es Salaam leo wakati Diwani wa Kata hiyo Mohamed Msophe (kulia) wa kwanza alipowasilisha taarifa ya utekelezaji wa ILANI kwa kipindi cha 2019/2020(PICHA NA HERI SHAABAN)
 Diwani wa kata ya Kipunguni Wilayani Ilala Mohamed Msophe akisoma taarifa ya Utekelezaji wa ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kipindi cha Mwaka 2019/2020 Dar es Salaam leo (Kushoto) Katibu Mwenezi wa CCM wa Kata hiyo Magige Chacha na Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipunguni Joven Chalange (PICHA NA HERI SHAABAN)
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Kipunguni Wilayani Ilala Joven Challange akizungumza na viongozi wa CCM wa Kata ya Kipunguni Dar es Salaam leo wakati Diwani wa Kata hiyo Mohamed Msophe (aliyekaa) alipokuwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani kwa kipindi cha 2019/2020 (PICHA NA HERI SHAABAN)

NA HERI SHABAN

DIWANI wa Kata ya Kipunguni (CCM) Mohamed Msophe amesoma taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi 2019/2020

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani Dar es Salaam leo Mohamed Msophe alisema kata ya Kipunguni ni miongoni mwa kata 36 manispaa ya Ilala.

Alisema katika kipindi cha 2018/2019 Idara ya Maendeleo ya jamii katika utekelezaji wa ILANI ya chama kupitia sekta ya mikopo ilifanikiwa kutoa mikopo ya riba nafuu asilimia 10 katika kila mtaa na kata ya Kipunguni.

"Katika kata yangu Vikundi kumi viliomba mkopo watu 50 kwa kila sekta MTAA wa Kitinye, Mtaa wa Machimbo,Mtaa wa Amani, Kipunguni B katika mitaa hiyo vikundi vilivyo bahatika kuchukua mikopo hiyo ya serikali vikundi 74"alisema Msophe.

Msophe alisema katika vikundi hivyo Wanawake 324 vijana wa kiume 26 katika vikundi hivyo mkopo uliotolewa shilingi, 143,500,000 wote kwa sasa Wapo katika hatua ya marejesho.

Msophe alisema katika utekelezaji wa ILANI pia amekabidhi vikundi vinne kila kikundi kuku 50 ili wajishughulishe.

Akielezea sekta ya elimu alisema wameongeza madarasa mawili,wamenunua mashine ya kudurufu mitihani ya majaribio shuleni
Kwa ajili ya wanafunzi kujipima baina ya shule kwa shule.

Aidha alisema mpaka sasa kuna vikundi vingine vipya 40, vimeshakamilisha usajili Halmashauri ya Ilala vinasubiri kuchukua mikopo ya Manispaa ya Ilala isiyo na riba, kwa ajili ya vikundi vyao na Miradi ya pamoja.

Pia alisema Watoto wa mitaani 45 wanajifunza Elimu ya ushonaji Kituo cha Sauti ya Jamii Kipunguni mafunzo ya kushona bure.

Akielezea sekta ya Maji kupitia serikali miradi iliyotekelezwa visima vinane kati ya visima vinane vitano ndio vinatoa maji kwa wananchi.

"Katika utekelezaji wa ILANI ya chama pia ofisi yangu imewalipia masomo VIJANA 15 mafunzo ya Cherahani katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kati ya wanafunzi hao wanne wamemaliza masomo wamepatiwa Cherahani kila moja kama sehemu ya ajira yao.

Kwa upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi wa kata hiyo Magige Chacha aliwataka wana CCM kuacha nongwa na chokochoko na Wanachama watakaonza kampeni watashughukiwa na chama

Aliwataka wanachi wa Kata ya Kipunguni kushirikiana na serikali katika kufanya kazi na kuleta maendeleo.

Mwisho
Share To:

Post A Comment: