Gari la abiria lenye namba za usajili T930 DML aina ya Toyota Coaster lililobeba wanafunzi wa sekondari limegonga Treni eneo la Kwamichi Jijini Tanga na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi.

Basi hilo lililokuwa limebeba wanafunzi wachezaji pamoja na washangiliaji zaidi ya 30 liliweza kuburuzwa umbali wa mita 50 kutoka eneo ilipotokea ajali .

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe akizungumzia ajali hiyo iliyotokea jana Ijumaa Machi 15, 2019 amemtaja aliyefariki katika ajali hiyo kuwa ni kondakta wa basi hilo ambaye jina lake halijatambulika mara moja.

Majeruhi waliofikishwa hospitali ya Mkoa wa Tanga ya Bombo ni wanafunzi 30 ambapo 19 kati yao hali zao si nzuri na madaktari wanaendelea na kuwapa matibabu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: