Monday, 18 March 2019

BREAKING: Maalim Seif ajiunga na ACT Wazalendo


Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Maalim Seif leo Marchi 18, 2018 ametangaza kujiunga na Chama cha ACT Wazalendo.

Hii ni baada ya Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba kutimua kiongozi hiyo siku mbili zilizopita.

"Shusha tanga, pandisha tanga safari iendelee,' amesema Maalim Seif wakati akitangaza uamuzi huo.

Utakumbuka mapema leo Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imekubaliana na uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini wa kumtambua Prof. lbrahimu Lipumba kuwa Mwenyekiti halali wa Chama cha Wananchi CUF.

Aidha imetupilia mbali maombi yaliyofunguliwa na Maalimu Seif Sharifu Hamad aliyeomba mahakama kutoa amri ya kubatilisha barua ya Msaji|i wa Vyama ya kumtambua Profesa Lipumba kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho

No comments:

Post a comment