Majid AbdulKarim

Waziri wa Nchi Ofisi , Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Seleman
Jafo ametoa wito kwa wananchi wa Kata ya Swaswa, Manispaa ya Dodoma kuchangamkia fursa
ya ujasiriamali katika kipindi cha ujenzi wa barabara ya Martin Luther kuelekea Swaswa yenye
urefu wa kilomita moja nukta tisa (1.9km).


Wito huo ametolewa leo katika ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu ya barabara katika Jiji
la Dodoma ambapo amewataka Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA), kukamilisha
barabara hiyo ndani ya mwezi moja kuanzia sasa.
Aidha Mhe. Jafo amesema ujenzi wa mradi huo ni neema kwa wakazi wa eneo hilo ambapo
watapata fursa ya kuwa na migahawa kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali za kijamii kwa
wananchi watakao kuwa wakifanya kazi katika mradi huo ili kujipatia kipato kitakacho wainua
kiuchumi.

‘Mungu akijalia tarehe 21 mwezi Desemba mwaka huu ntakuwepo hapa saiti kukagua kama
mradi huu umekamilika kwa wakati na uko katika ubora unaohitajika’’ alisema Jafo.
Mhe. Jafo meongeza kuwa TARURA wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia wakandarasi wa
barabara zote zinazojengwa nchini kuwa zinajengwa kwa kiwango kinacho hitajika ili ziweze
kutumika kwa muda uliopangwa.
‘Nimeridhika na ujenzi wa barabara ya TPS, upo katika hatua mbalimbali na ujenzi unaenda
vizuri nimejionea mpaka sasa na wameniambia ujenzi huu uko katika asilimia 20’’ Alisema Mh.Jafo .

Naye Mkuu ya Wilaya wa Dodoma Mjini, Mhe. Patros Katambi amesema jukumu lake ni
kuhakikisha anatekeleza maagizo yote yanayotolewa na viongozi wake wa ngazi za juu kwa
kushirikiana na viongozi wake wa ngazi ya wilaya.
Mkazi wa Swaswa, Bi Anna Charles amesema ujenzi wa barabara hiyo ukikamilika itakuwa ni
kheri kwa wakazi hao kwani itaondoa adha ya usafiri kwa sababu wamekuwa wakitembea
mwendo mrefu kutafuta usafiri.
Bi. Anna ameendelea kwa kusema kuwa itaondoa usumbufu kipindi cha mvua barabara hiyo
imekuwa haipitiki kutokana na barabara hiyo kujaa maji kipindi cha mvua.
Mradi huu wa ujenzi wa barabara ya Martin Luther unatakiwa ukamilike ndani ya mwezi mmoja
kuanzia sasa na kukabidhi 21 Disemba mwaka huu.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: