Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Wilaya ya Karatu ina kesi 19 za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari zilizofikishwa mahakamani ikiwa ni juhudi za kupambana na hali hiyo inayoongezeka kwa kasi kutokana na usiri katika familia za wahanga.

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Karatu Abdalah Nyange  amesema kuwa wamekua wakishirikiana na polisi pamoja na mahakama ili kutokomeza vitendo vya kikatili dhidi ya watoto wa like na kuhakikisha ustawi bora wa jamii.

Amesema kuwa licha ya kesi za mimba za utotoni pia kuna kesi za ubakaji na ukatili wa kijinsia ambazo wamezifikidha mahakamani ili watoto waweze kupata haki.

Kaimu Mratibu wa shirika la World Vision katika Mradi wa Endabash ,Rachael Pazia amesema kuwa lengo la mradi huo ni  Kupambana na mimba za utotoni pamoja ukeketaji hivyo shirika hilo limekua na mikakati mbalimbali ya kuwatetea watoto wa kike na kutoa elimu kwa jamii ili kuondokana na vitendo hivyo vinavyorudisha nyuma maendeleo ya watoto wa kike na jamii kwa ujumla.

Afisa Tawala Wilaya ya Karatu Jackline Rwezaula pamoja na Mwanafunzi wa shule ya sekondari Endabash  Patricia Laurian  amesema kuwa watoto wa kike wanapaswa kushinda vishawishi ili kutokomeza mimba za utotoni ambazo zimekua ni changamoto kubwa kwa jamii nyingi za wafugaji.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: