Friday, 19 October 2018

Wajasirimali na wataalum 800 wa Tiba na Dawa Baridi Kanda ya Ziwa wakutana Nyamagana kunolewa


Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kushirikiana na  Mkuu wa mkoa Mwanza pamoja na Halmashauri ya Jiji la Mwanza yawakutanisha wajasirimali, wataalumu wa Tiba na Dawa"Pharmacist"  800 kutokea mikoa ya Kanda ya Ziwa katika semina elekezi kwa siku tatu kwanzia 15-19/10/2018  Wilayani Nyamagana.

Semina hii elekezi ni mkakati wa Wizara katika mpango wake kabambe kuwajengea uwezo watoa huduma na wamiliki wa Maduka ya Dawa baridi kibiashara kupitia mafunzo ya ujasirimali, uchambuzi wa sheria, taratibu pamoja na kanuni mbali mbali za uendeshaji wa biashara.

Mafunzo haya kwa Kanda ya Ziwa yameendeshwa na Mkufunzi George Marwa pamoja na Tibaijuka kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ndg. Antoni Yesaya kutokea Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza pamoja na  Ndg. Halidi Mashashi kutokea Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿

No comments:

Post a comment