Maafisa wanaosimamia madawati ya mikopo vyuoni wametakiwa kutokuwa chanzo cha migogoro ili kuhakikisha wanafunzi wanapata huduma bora isiyokuwa na urasimu, kuacha umangimeza, rushwa na badala yake wahakikishe wanaimarisha madawati yao ili kuhakikisha wanafunzi wenye sifa na uhitaji   wanufaika na mikopo kama ilivyokusudiwa na Serikali.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa James Mdoe wakati akizungumza katika kikao kazi cha siku mbili  cha maafisa hao kilichoanza leo mjini Bagamoyo na kusisitiza kuwa dhamira ya Serikali ya awamu ya Tano ni kuhakikisha watanzania wengi wanapata Elimu ya juu.
Profesa Mdoe amesema kwa mwaka wa fedha 2018/19  serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 427. 5 ambapo jumla ya wanafunzi 124 watanufaika na mkopo huo, na kuwa ugawaji wa mikopo hiyo uzingatie haki, vigezo, kanuni na sheria.
“ Nataka twende vizuri tukahakikishe huduma bora inatolewa katika mwaka huu mpya wa masomo ikiwa ni pamoja kutoa huduma bora,kusimamamia kumbukumbuku na kuhakikisha mawasiliano ya mara kwa mara yanakuwepo  kati ya maafisa mikopo na bodi ya mikopo na kwa haipendezi maafisa mikopo kuwa chanzo cha migogoro,”amesisitiza Profesa Mdoe.
Profesa Mdoe pia ameitaka bodi hiyo  kuimarisha  mifumo ya TEHAMA ili kuboresha utendaji kazi, ikiwa ni pamoja na kuongeza kasi ya kuwasaka waajiri  warejeshe fedha ambazo wafanyakazi wao walisoma kwa mkopo, ili fedha hizo zitumike kwa wanafunzi wengine.
Akizungumza katika kikao kazi hicho Mkurugenzi Mtendaji wa bodi ya mikopo Abdul- Razq badru amesema kuwa maagizo yote yaliyolewa na Naibu katibu Mkuu watayasimamia katika utekelezaji wa ugawaji wa mikopo kwa wnanafunzi huku akikiri kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wa mikopo hiyo inayotolewa na serikali.
“Bdodi ya mikopo inaahidi kusimamia haki, vigezo, kanuni na sheria katika utoaji wa mikopo hiyo kwa wanafunzi kama ambavyo sheria zinavyoelekeza, niwasihi sana maafisa mikopo kufanya kazi kwa weledi na kuacha mazoea ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza,”alisisitiza Badru

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA
12/10/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: