Saturday, 13 October 2018

SALUM KALLI AFUNGUA RASMI KONGAMANO LA KUMUENZI BABA WA TAIFA KATA YA MBUGANIKatibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum Kalli amefungua kongamano la kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere Kata ya Mbugani  kwa kumbukizi za miaka 19 toka atangulie mbele za haki ambapo maadhimisho haya kitaifa kufanyika Mkoani Tanga.

Ndg. Kalli ametumia adhara hiyo kuasa wana Nyamagana na wana Mbugani kuangalia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika taifa la Tanzania kwa kupima maendeleo yalivyojijenga kwanzia awamu ya kwanza hadi  awamu ya tano.  Kutumia historia ya mafanikio kwa kumuenzi mwasis wa taifa hili Hayati Baba wa Taifa Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa moyo wa uzalendo, uwajibikaji na kwa kuiunga mkono serikali ya CCM iendelee kuongoza taifa hili kwani, ndio Chama pekee cha Siasa chenye mfumo imara na Sera madhubuti zenye tija katika mstakabali wa maendeleo ya taifa la Tanzania.

Kongamano hili la siku moja limehudhuriwa na mjumbe mkutano mkuu taifa Samson Ng'warida, Katibu Hamasa na Chipukizi mkoa wa Mwanza Ndg Hussein Kimu, Viongozi waandamizi wa chama Cha Mapinduzi Kata wakiomgozwa na Kamati ya Siasa, Diwani mwenyeji Mhe. Gombe Gombe, wajumbe Halmashauri ya CCM kata pamoja viongozi Matawi ya CCM Matatu, wazee maarufu, Wenyeviti wa mitaa pamoja na Balozi wa Nyumba kumi kumi. Na kuwa na  mchokoza Mada Waalimu wabobezi katika maswala ya itikadi na Siasa Ndg. Salum  Kalli aliyefundisha Medani za ushindi wa Uchaguzi, Ndg. Salum Neja akiwasilisha mada ya Majukumu na mipaka ya uongozi pamoja na maadili na sifa ya uongozi.

Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi
Wilaya ya Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: