Jeshi la polisi mkoani Shinyanga limefanikiwa kukamata gari lenye namba za usajili T.613 DDH Toyota Hiace mali ya Martine Henerico (57) lililoibiwa katika kituo kidogo cha magari cha Phantom mjini Shinyanga. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Oktoba 12,2018 Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa amesema gari hilo ambalo liliibiwa tarehe 20 Agosti 2018 katika Stendi ya Phantom Mjini Shinyanga lilikamatwa eneo la Igoma jijini Mwanza Septemba 24,2018.

“Mtuhumiwa Fanuel Salum Sumbayi (34) tayari amefikishwa mahakamani kwa hatua kali za kisheria,alibadili namba za gari T613 DDH na kuwa T.618 BDN”,ameongeza Mutalemwa.

Amesema jeshi la polisi pia limekamata gari lenye namba za usajili T.428 CF Q Toyota Premio ambalo linadaiwa kutumika kufanya utapeli katika maeneo ya mkoa wa Shinyanga,Mwanza na Dar es salaam ambapo juhudi za kumkamata mmliki wa gari hilo zinafanyika ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Ameongeza kuwa pia wamefanikiwa kukamata pikipiki 18 zilizoibiwa kwa watu mbalimbali mkoani Shinyanga na darubini nne ‘Student Microscope’ alizokutwa nazo Emmanuel Kazimili (29) ambazo zinadaiwa kuwa za wizi.

Katika operesheni,misako na doria za jeshi hilo, zimekamatwa dawa za kulevya aina ya bangi kilo 120,heroine gram 60,pombe za kienyeji ‘Moshi’ lita 200,mitambo 11 ya kutengenezea pombe ya moshi na jumla ya watuhumiwa 57 wamefikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha namba za usajili za hiace iliyoibiwa ambapo baada ya kuibiwa Mtuhumiwa Fanuel Salum Sumbayi alibadili namba za gari T613 DDH na kuwa T.618 BDN. Picha zote na Kadama Malunde1 blog
Namba za gari T613 DDH zikiwa zimebadilishwa na kuwa T.618 BDN.
Gari lenye namba za usajili T.613 DDH Toyota Hiace mali ya Martine Henerico (57) lililoibiwa katika kituo kidogo cha magari cha Phantom mjini Shinyanga ambalo limekamatwa jijini Mwanza. 
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha  gari lenye namba za usajili T.428 CF Q Toyota Premio ambalo linadaiwa kutumika kufanya utapeli katika maeneo ya mkoa wa Shinyanga,Mwanza na Dar es salaam ambapo juhudi za kumkamata mmliki wa gari hilo zinafanyika. 
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha pikipiki 18 zilizoibiwa kwa watu mbalimbali mkoani Shinyanga.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha pombe ya moshi na mitambo ya kutengenezea pombe hiyo.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha gunia la bangi.
Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Alchelaus Mutalemwa akionesha moja kati ya darubini nne zinazodhaniwa kuwa za wizi aliozokamatwa nazo Emmanuel Kazimili.
Picha zote na Kadama Malunde1 blog
Share To:

Anonymous

Post A Comment: