Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanislaus Mabula amewaambia wananchi wa Kata ya Mabatini kupitia mkutano wa hadhara viwanja vya Kabengwe, serikali ya Chama Cha Mapinduzi kupitia Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeweka mkakati wa kukabiliana na changamoto za upungufu wa vyumba vya Madarasa 1200 inayoikabili sekta ya elimu katika shule za sekondari na Msingi Wilayani Nyamagana.  *Tumenunua kifyatulio cha Tofari chenye uwezo wa kufyatua Tofari 6000 kwa Saa, tutaagiza Saruji na Nondo kutoka kiwandani tukitazamia ifikapo 2019 tutakamilisha ujenzi wa Vyumba vya madarasa 1200* Mhe Mabula amesema.

Mhe. Mabula akijibu hoja ya Diwani Mteule wa Kata hiyo Ndg. Deo Lukas aliyepitwa bila kupingwa katika uchaguzi wa marudi wa kata hiyo na kutarajiwa kuapishwa mnamo tarehe 13.10.2018, amehaidi kukarabati Vyumba vitano vya madarasa Shule ya Msingi Mabatini kupitia mfuko wa Jimbo.

Mkutano huu wa hadhara umehudhuliwa na Viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi wakiongozwa na Katibu CCM wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum Kalli, Diwani Mteule Kata ya Mabatini, Diwani Kata ya Nyegezi Mhe Edith Mudogo, Diwani Viti Maalum Mariam Mafuta na Anifa Mhere, watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Share To:

msumbanews

Post A Comment: