Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanislaus Mabula ametembelea mradi mkubwa unaotekelezwa na taasis ya SOS kwaajili ya ujenzi wa Vyumba saba vya madarasa shule ya Msingi Igelegele Kata ya Mahina uliogharimu shilingi 255,000,000.00. *Kwa dhati nawapongeza wadau wa maendeleo SOS kwa ujenzi wa Vyumba vya madarasa vizuri, vyenye ubora na vinavyozingatia matumizi bora ya Ardhi na kufanya shule ya Msingi Igelegele kuwa shule ya kwanza ya serikali Nyamagana  yenye majengo mazuri baada ya shule ya Nyanza*.Mhe Mabula amesema.

Naye Kaimu maneja wa taasis ya SOS Ndg. Samson amesema taasis yake imedhamiria kuboresha huduma ya elimu Wilayani Nyamagana, ikiwekeza zaidi Shule ya Msingi Igelegele ili iwe miongoni mwa Shule ya mfano katika halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa ubora wa majengo na huduma. Katika awamu ya kwanza SOS ilijenga vyumba vya madarasa vipya na kukarabati madarasa chakafu pamoja na ujenzi wa matundu ya vyoo. Katika awamu ya pili ya mradi utawezesha kumaliza uhaba wa vyumba vya madarasa shule hapo.

Mhe. Mabula ameambatana na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata na Tawi, Mtendaji wa Kata na Mtaa pamoja na ujumbe wa taasis ya First Community Organization.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿




Share To:

msumbanews

Post A Comment: