Thursday, 11 October 2018

Makonda Apiga Marufuku Mabasi ya Mwendo Kasi Kuacha Abiria Vituoni....Pia Kawaruhusu Abiria Kupiga Picha

Mkuu wa Mkoa wa Dar es SalaamPaulMakonda amesema ni marufuku kwa dereva yeyote wa mabasi yaendayo kasi kuacha abiria vituoni. Mabasi hayo ni yale ya ‘Express’ ambayo husimama vituo maalumu pekee.

Makonda ametoa kauli hiyo leoalipotembelea kituo cha mabasi cha Kimara na kusikiliza kero za wananchi.

Baada ya kusikiliza kero za abiria katika kituo cha Kimara-Mwisho, Makonda amesema haoni sababu ya madereva kuacha kuchukua abiria vituoni kwa sababu ni Express.

"Nimeshaongea na viongozi, hakuna haja ya gari kupita kwenye kituo na kuacha abiria. Kuanzia sasa hivi wanaotoa huduma za usafiri hakuna abiria kuachwa njiani," amesema.

Makonda amesema usafiri huo ulianzishwa kwa lengo la kurahisisha shughuli kwa wananchi na si kuwachelewesha kama hali ilivyo hivisasa.

Katika hatua nyingine, RC  Makonda amesema ni  ‘ruksa’ kwa abiria wa mabasi yaendayo kasi kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo.

Licha ya katazo la kupiga picha kwenye vituo vya mabasi hayo, Makonda amewataka abiria kuwa huru.

Makonda amesema abiria wapige picha ili kuwafichua watoa huduma wavivu na wanyanyasaji.

Amesema ndani ya siku tatu ufumbuzi wa kudumu juu ya kero za usafiri utapatikana.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: