Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Leonard Akwilapo amewataka washiriki wa mafunzo ya Force Akaunti kuhakikisha wanazingatia Kanuni, taratibu na Sheria wakati wa usimamiaji wa ujenzi na ukarabati  wa miradi ya serikali.

Dkt. Akwilapo ametoa kauli hiyo wakati akifunga mafunzo ya siku mbili ya matumizi ya Force Akaunti yanayofanyika mkoani Morogoro ambayo yameshirikisha  watumishi wa Serikali wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakurugenzi wa kanda VETA, Maafisa Kutoka  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Maafisa kutoka VETA.

Katibu Mkuu huyo amewaeleza washiriki hao kuwa utaratibu wa Force Akaunti upo kisheria, hivyo amewasisitiza washiriki kuhakikisha wanakuwa na utunzaji wa kumbukumbu ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa risiti za kielektroniki (EFD).

Dkt. Akwilapo  amesema kuwa Force Akaunti ikisimamiwa vizuri inaonyesha thamani ya Fedha, mradi unakamilika na kuwa yote hayo yanawezekana enadapo  ushirikiahwaji na uwazi miongoni mwa Jamii utakuwepo katika eneo ambalo mradi unatekelezwa.

Mafunzo hayo ya siku mbili yanaratibiwa na mradi wa kukuza Maarifa, Stadi na ujuzi (ESPJ) yamehusisha Wakurugenzi wa halmashauri za Kasulu,Ngorongoro,Kongwa,Nyasa, Wakurugenzi wa  Kanda VETA, Wakurugenzi wasaidizi kutoka Makao Makuu VETA na Maafisa kutoka VETA,

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA
2/10/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: