Saturday, 20 October 2018

DC KATAMBI NA MBUNGE MAVUNDE WASIKILIZA NA KUTATUA KERO ZA WAENDESHA BAJAJ NA BODABODA JIJI LA DODOMA

index
Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh Patrobas Katambi pamoja na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh Anthony Mavunde leo wamesikiliza na kutatua kero za maelfu ya waendesha bajaj na bodaboda wanaofanya shughuli zao katika Jiji la Dodoma.
Viongozi hao wameahidi kuwa bega kwa bega na waendesha bajaj na bodaboda kwa kuwataka kuanzisha UMOJA wenye nguvu ili waweze kuwawezesha kupitia fursa mbalimbali za mikopo,huku DC Katambi akisisitiza utii wa sheria bila shurti na kulitaka Jeshi la Polisi kuanzisha dawati maalum la kushughulikia matatizo ya waendesha bajaj na bodaboda.
Wakati huo Mbunge Mavunde ameahidi kuwananulia UMOJA huo samani za ofisi,computer na mchango wa Tsh 1m kutunisha mfuko wa Umoja huo.
Mkutano huo mkubwa ulifanyika katika uwanja wa Jamhuri Dodoma ulihudhuriwa pia na Viongozi wa Jeshi la Polisi,TRA,NHIF na SUMATRA ambao wote walipata nafasi ya kutolea ufafanuzi baadhi ya malalamiko yaliyoelekezwa katika taasisi zao.

No comments:

Post a comment