Monday, 8 October 2018

ARUSHA UNITED YATAMBA KUSHINDA MCHEZO NA NDUGU ZAO AFC


Na Ahmed Mahmoud Arusha,
Timu ya soka ya Arusha United SC,(WANA UTALII) ya mkoani hapa imetamba kushinda mchezo wake na nduguzao wa Arusha Football Club(AFC) katika mchezo wao utakaopigwa tarehe 20 mwezi huu katika dimba la Sheikh Amri Kaluta Abeid jijini hapa.
Akizungumza na vyombo vya habari Msemaji wa Timu Hiyo Jamila Omary amesema kuwa wamejipanga kushinda mchezo huo kujihakikishia pinti tatu muhimu kabla hawajatoka kwenda kucheza michezo ya ugenini.
Jamila Amesema kuwa uwezo wanao na nia ya kuwafunga wanayo hivyo wakazi wa Arusha waje kujionea burudani katika mchezo huo ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka mkoani hapa.
“Nia ya kuwafunga Afc tunayo uwezo tunao kwani kikosi chetu ni imara tunasubiria mchezo huo kwa hamu kubwa ya ushindi asubuhi kweupe lazima walale AFC”alijigamba msemaji huyo.
Nae kocha mkuu wa Arusha United Fred Felix Minziro”Majeshi” amesema kuwa wachezaji wake wapo katika hali nzuri na timilifu kusubiria mchezo huo ambapo hakuna majeruhi wowote hadi sasa na wanaendelea na mazoezi kujiwinda na mchezo huo na ana uhakika wa kushinda mchezo huo ilikujiweka vizuri kupanda ligi kuu mwakani.
Kwa upande mwingine katibu mkuu wa timu ya AFC Lyimo amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa tarehe 20 mwezi huu kwani mchezo huo wanauchukulia kwa tahadhari kubwa kuongeza pionti.
Amesema kuwa timu hizo ambazo zote zipo kundi D katika ligi daraja la kwanza zimekuwa ni sehemu ya kuhakikisha mkoa wetu unakuwa na timu ya ligi kuu mwakani hivyo wamejipanga teyri tuna pinti mbili tulizopata ugenini.
Mchezo huo ambao ni Derby ya jiji la Arusha utahudhuriwa na mashabiki na viongozi mbali mbali wa soka mkoani hapa na jirani umekuwa ni kuvutio baada ya kila timu kutamba kushinda mchezo huo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: