MKAZI wa Mikocheni A, Pyana Herbo (45), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni, Dar es Salaam kwa tuhuma za kumshambulia kwa mchapa fimbo mtoto.

Karani wa Mahakama hiyo, Januari Kasekwa alidai mbele ya Hakimu Marko Mochiwa kuwa Septemba 10 saa 4 asubuhi eneo la Mikocheni A, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alimshambulia mtoto Christina Hebron kwa kumpiga na fimbo sehemu mbalimbali za mwili.

Mshtakiwa alikana shtaka hilona alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana hadi Oktoba 5, mwaka huu, kesi itakapotajwa tena.

Na ZAKIA NDULUTE (UoI) Na HAPPYNESS GRAYSON (UoI) | 
Chanzo- Mtanzania
Share To:

Anonymous

Post A Comment: