Tuesday, 9 October 2018

150 MIL KUTUMIKA KUJENGA ZAHANATI KATA YA MHANDU NYAMAGANAHaya yamebainika katika ziara maalum ya Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza Ndg. Kiamoni Kibamba kutembelea ufyatuaji wa tofari za  hydro form zitakazotumika kwenye mradi wa ujenzi wa zahanati Kata ya Mhandu. Ujenzi huu wa Zahanati unatarajiwa kuanza tehere 12.10.2018 siku ya ijumaa na kugharimu takribani shilingi 150,000,000.00.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Kata ya Mhandu Mhe. Constantine Sima ameipongeza serikali ya Chama Cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais wa awamu ya tano Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kuwezesha ujenzi huo, ili kutatua changamoto za upatikanaji wa huduma ya Afya kwa kusogezea wananchi huduma Karibu.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mwanza katika ziara hii amemabatana na Manejiment ya watumishi wa jiji la Mwanza.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: