Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia leo imewajengea uwezo Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendelo ya Jamii kwa kuwasilisha  majukumu  14 yanayoyekelezwa na Wizara hiyo kwa mujibu wa hati idhini iliyotolewa April 22, 2016.

Akiwasilisha majukumu hayo Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango Makuru Petro ametaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na kutunga na kutekeleza Sera za Elimu, utafiti,Huduma za Maktaba, Sayansi na Teknolojia na uendelezaji wa mafunzo ya Ufundi, kuendeleza Elimu kwa kutoa ithibati ya mafunzo ya Ualimu na Maendeleo y kitaalamu ya Walimu, Kusimamia uendelezaji wa mafunzo katika vyuo vya Maendeleo ya wananchi, na kusimamia mfumo wa  tuzo wa Taifa.

Majukumu mengine ni kuainisha mahitaji ya nchi katika ujuzi,kuweka viwango vya Taaluma ya Ualimu ikiwemo kuanzisha bodi ya kitaalamu ya walimu, kusimami ithibati na uthibiti ubora wa shule kwa kuweka viwango, kusimamia Huduma za machapisho yakielimu ikiwemo mitaala na vitabu, kuimarisha utumiaji wa Sayansi, Teknolojia na hisabati, kuendeleza wataalamu wa ndani katika Sayansi na Teknolojia, kuratibu na kusimamia utafiti, ubunifu katika fani za Sayansi na Teknolojia, kusimamia Tume ya Taifa ya UNESCO, uendelezaji wa Rasilimali watu na kuratibu shughuli za Idara, mashirika, wakala,programu na miradi iliyochini ya Wizara.

Kupitia uwasilishaji wa majukumu hayo ya Wizara wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara hiyo Wakuu walioata fursa ya kujibu maswali mbalimbali yaliyoizwa na Wabunge kwa lengo la kupata uelewa.

Taasisi zilizoshiriki katika kujibu maswali mbalimbali ya Wabunge ni pamoja na Bodi ya Mikopo ya  Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, (NACTE),Tume ya vyuo Vikuu Tanzania, (TCU),Taaaisi ya Elimu Tanzania (TET).

Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNLOJIA
11/9/2018
Share To:

msumbanews

Post A Comment: