Friday, 28 September 2018

Wananchi Mkoani Songwe wahimizwa kujitokeza kwa wingi kupima afya zao kuelekea siku ya Furaha yangu
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brig.Jen. Nicodemas Mwangela , amewataka wananchi wa Mkoa  huo  kujitokeza kwa wingi ili waweza kupima afya zao ili waweze kuishi kwa raha na amani.

Rc Mwangela ametoa kauli hiyo kuelekea kilele cha Siku ya Furaha Yangu itakayofanyika siku ya kesho Sept. 29/ 2018 katika Viwanja vya Shule ya sekondari Nalyelye katika Mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo  ambapo amewataka  wananchi kujikotoza kwa wingi katika kampeni hiyo ya Kitaifa ya kupima Virusi vya Ukimwi na kuanza kutumia vidonge vya kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi
 ( V V U ), Ijulikanayo kama Furaha Yangu, Pima, Jitambue, Ishi.

BONYEZA PLAY HAPO CHINI KUMSIKILIZA RC MWANGELA.

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: