Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (kulia) akizungumza na wanachama wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, wakati wa yeye na timu yake walipofanya ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji unaotekelezwa na skimu hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine (aliyenyanyua mkono) akipata maelezo ya maendeleo ya matrekta na mashine ya kuvunia walizozitoa kama mkopo kwa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga.
 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akichukua kumbukumbu ya mandhari ya shamba lenye ukubwa wa hekta 220 linalolimwa kwa ufadhili wa mkopo kutoka TADB.
 Timu ya Ukaguzi ikiangalia mandhari ya mifereji inayotumia kumwagilia shamba hilo.
 Timu ya Ukaguzi ikiangalia namna uongezaji wa thamani wa zao la mpunga unavyofanyika,
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine akioneshwa mfuko utakaotumika kufungashia mchele unaozalishwa na Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo. Skimu hii imeweshwa kwa mkopo unaotolewa na TADB


Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, (TADB) imeahidi kunyanyua kipato cha wakulima wadogo wadogo kupitia ushirika wao kwa kuwapatia mikopo ya gharama nafuu ili waweze kumudu gharama za uzalishaji.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa mradi wa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji katika Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo iliyopo mkoani Tanga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake imejidhatiti kuwasaidia wakulima wadogo wadogo nchini kwa kuwapatia mitaji itayowawezesha kununua zana bora za kilimo ili kuweza kuongeza uzalishaji kama ilivyoanishwa katika Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Kilimo (ASDP 2).

Akizungumza kwa niaba ya wakulima wa skimu hiyo, Katibu wa Skimu ya Umwagiliaji ya Mombo, Bwana Sufian Mohamed aliishukuru serikali kupitia Benki ya Maaendeleo ya kilimo kwa kuwapatia mkopo wa gharama nafuu ambao umeweza kuwanufaisha jumla ya wakulima 429 kati yao wanawake wakiwa asilimia 54, mkopo ambao umeboresha miundo mbinu ya skimu hiyo hali iliyowezesha kuongeza uzalishaji kutoka wastani wa tani 1.9 hadi kufikia tani 6 kwa hekta moja.

Skimu hiyo ya Mombo mpaka sasa imenufaika na mkopo wa mbolea, mbegu bora pamoja na trekta, mashine ya kuvunia na sasa Benki ya Kilimo ipo katika hatua ya mwisho ya kuwapatia mashine ya kukobolea mchele ili waweze kuongeza thamani ya zao la mpunga katika skimu hiyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: