Saturday, 1 September 2018

Sababu ya ongezeko la migogoro ya ardhi Tanga yatajwa


Migogoro ya ardhi wilayani Korogwe mkoani Tanga imedaiwa kuchangiwa na ongezeko la watu pamoja na mifugo, hali iliosababisha baadhi ya wadau kuiomba serikali kuendelea kupambana na tatizo hilo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira wa halmashauri ya wilaya ya Korogwe amesema hayo muda mfupi baada ya kuwasilisha taarifa yake mbele ya watumishi wa idara mbalimbali pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo.

Amesema matatizo hayo pia yamejitokeza hata kwenye maeneo ya mipaka ya wilaya hiyo na zile inazopakana nazo kutokana na wananchi kutotambua mipaka hiyo, hali inayosababisha muingiliano hasa kwenye maswala ya kilimo na malisho.

Hata hivyo, serikali tayari imeanza jitihada za kukabiliana na changamoto hizo na wananchi wametakiwa kuwa na subira.

Halmashauri ya wilaya ya Korogwe imetenga eneo la Mnyuzi kuwa kwa ajili ya makazi hatua ambayo pia inaweza kusaidia kupunguza changamoto ya ardhi wilayani humo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: