WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi pamoja na Waziri wa Mifugo  na Uvuvi Luhaga Mpina kwa pamoja  wamemaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu katika eneo la Pugu Stesheni na Bangulo na kuwakabidhi eneo la hekari 1792  walilokuwa wamevamia.

Akitoa maamuzi hayo Waziri mwenye dhamana ya mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina mbele ya wananchi hao amesema kuwa amekubali kuwapa eneo hilo huku akiwataka wananchi hao kutovamia hekari 108 zilizobaki  kwani zitaendelea kuwa za serikali.

Hayo ameyasema Mpina hapa katika eneo la pugu mnadani ambapo mkutano mkuu wa kuwakabidhi ulifanyika hatua iliyoibua vifijo na vigelegele kutoka kwa wananchi hao.

" Nasema nimekubali kuwapa  hekari ,1792 lakini nawaomba hekari 108 zilizobaki wasizivamie tena na yeyote atakayefanya hivyo hatavumiliwa kamwe na atakuwa ameingia kwenye mgogoro mkubwa na serikali."alisema Mpina

Pia baada ya kutoa maamuzi hayo Luhaga mpina aliwataka wananchi  hao kuendelea kuishi kwa amani na upendo na kuheshimu na eneo lililobaki litapimwa na kubadilisha matumizi nakuwaeleza wananchi hao kuwa wanasalimiwa na Rais Dkt John Magufuli.

Kwaupande wake Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akizungumza katika mkutano huo alisema wao kimsingi wamekubaliana na hilo na watakachofanya nikuangalia eneo lingine la kupeleka mnada huo.

Amesema baada ya kuwapa eneo hilo hatua inayofuata nikubadilisha hati kutoka kwenye miliki ya Serikali na kutoa kwa wananchi hao.

"Nasema kuwa hatua Inayofuata ni wanachi hao kutengeneza kamati ambayo itashughulikia upatikanaji wa hati miliki na kuweza kurasmishwa rasmi."alisema Lukuvi

Lukuvi alisema wao kama serikali baada ya wananchi hao kukamilisha taratibu zote watakuja kupanga miundombinu yake ikiwamo kuweka mitaa,maji,na mambo mengine .

Kwa upande wake RC wa Dar es Salaam Paul Makonda amewashukuru mawaziri hao kwa jitihada kubwa walizofanya jambo ambalo limemfanya aone thamani kama Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa.

Amesema wamefanya kazi kubwa na kinachoendelea nikutatua changamoto hizo za migogoro ya ardhi katika maeneo.mengine katika jiji la Dar es Salaam.
Share To:

Post A Comment: