Wednesday, 12 September 2018

RC GAMBO APOKEA MWENGE WA UHURU, WAANZA KUZINDUA MIRADI WILAYA YA NGORONGORO
Mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima akimkabidhi mwenge wa uhuru Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka Gambo katika eneo la makumbusho Olduvai Gorge wilayani Ngorongoro.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndg: Charles Francis Kabeho akizundua huduma za ugavi,udhibiti wa magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Nainokanoka wilayani Ngorongoro baada ya mwenge wa uhuru kukabudhiwa rasmi mkoa wa arusha septemba 12.


 Kutoka kulia ni Kiongozi mkuu wa mbio za mwenge wa uhuru Charles Francis Kabeho akiwa katika ukaguzi wa vifaa vya maabara katika shule ya sekondari Nainokanoka wilayani Ngorongoro kabla ya uzinduzi wa Jengo hilo.MKUU wa Mkoa wa Arusha Mrisho Mashaka  Gambo leo Sept. 12  amepokea Mwenge wa Uhuru uliowasili Asubuhi ya leo katika  eneo la makumbusho Olduvai Gorge wilayani Ngorongoro ukitokea Mkoa wa Mara na kuukabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro  kwaajili ya kuanza shughuli ya uzinduzi wa miradi ya maendeleo.

Uzinduzi wa mbio za mwenge wa uhuru 2018 ulianzia mkoani Geita April 2 mwaka huu na kilele ni siku ya kumbukumbu ya mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Oktoba 14 mwaka huu huko Mkoani Tanga.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: