Tuesday, 4 September 2018

Rais Magufuli Awamwagia sifa Wabunge wa CCM


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli jana  kwenye ziara yake Mkoani Mwanza akihutubia katika hafla ya utiaji saini mikataba ya ujenzi wa meli ya MV.Butiama na MV. Victoria amewapongeza wabunge wa CCM kwa kupitisha bajeti ya serikali na kuwananga wabunge kutoka vyama vya upinzani kwa kupiga kura ya hapana kwenye kuipitisha bajeti hiyo.

Magufuli alisema iwapo wabunge wa CCM wangepiga kura ya hapana kama wabunge wa upinzani serikali isingeweza kutekeleza miradi ya maendeleo ikiwemu wa ujenzi wa meli mpya unaotarajia kuanza hivi karibuni.

Alisema kuwa kura ya hapana maana yake watu wa Bukoba waendelee kupata tabu, watu wa Victoria wasiweze kufanya biashara na waendelee kuteseka kwa  kukosa usafiri ndani ya Ziwa Victoria.

Aidha, Rais Magufuli aliwapongeza wabunge wa CCM kwa kuwawakilisha vyema wananchi wa Bukoba na amawaomba waendelee hivyo hivyo.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: