Rais John Magufuli, amewataka mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za nje, kufanya kazi waliyotumwa au wajiandae.

Akizungumza baada ya kumwapisha Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro aliyemteua wiki hii baada ya kutengua uteuzi wa Dk. Susan Kolimba, amesema hatamvumilia balozi asiyefanya kazi.

“Kama kuna balozi atakwenda kule kunywa ‘wine’ miezi sita yote bila kufanya kazi ajiandae… wizara hii ina mambo ya ajabu sana Balozi wetu kule China, ameandika barua zaidi ya 24 zilizojibiwa ni mbili ndiyo maana nikaamua kutoa Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake,” amesema.

Kwa upande wake Dk. Ndumbaro amesema atakwenda kutekeleza kufanya kazi kwa mujibu wa maelekezo  aliyopewa.

“Nikuahidi rais nitakwenda kutekeleza maagizo hayo kwa mujibu wa maelekezo uliyotoa, nitatekeleza majukumu ya Katiba na kufuata Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukurasa 110 hadi 111 inayoongelea masuala ya kimataifa,” amesema Dk. Ndumbaro.
Share To:

Anonymous

Post A Comment: