Sunday, 2 September 2018

NYAMAGANA YAWA MWENYEJI WA UZINDUZI WA KAMPENI ZA SELI MUNDU/SIKO SELI KIMKOA


Mkoa wa Mwanza umezindua rasmi kampeni za mwezi wa uelewa wa Seli Mundu/ Siko Seli kimkoa Mosi Septemba. Kampeni hizi zimefunguliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg. John Mongella na kutarajiwa kufikisha ujumbe wa  *Vunja Ukimya  Tuongee Kuhusu Siko Seli* mkoa mzima.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mganga Mkuu amesema Seli Mundu au Siko Seli sio ugongwa wa kuambuzika bali ni miongoni mwa magonjwa ya kirithi. Serikali ipo katika michakato kuhakikisha ugonjwa huu unatoka katika magonjwa ya kurithi ifikapo 2020 hivyo jamii isiwanyanyapae wagonjwa wa Sikoseli.

Mratibu wa kampeni kimkoa Bi. Pascha Mazeze amesema Tanzania ni nchi ya tatu katika nchi za Jangwa la Sahara yenye watoto takribani 10,000 huzaliwa na Seli Mundu kila Mwaka.  Hivyo taasis ya TASIWA *Tanzania Sickle Cell Worriors* kwa kushirikiana na wadau wa Afya wamezindua kampeni hizi rasmi kwa matembezi kimkoa ambapo uzinduzi umefanyika wilaya ya Nyamagana nakutazamiwa kufika maeneo mbali mbali ya mkoa kwa mwezi mzima wa septemba ambao ni mwezi rasmi kimataifa.

Bi. Mazeze amesema matembezi hayo yamewakutanisha wahanga na wananchi wa matabaka na rika mbali mbali  kupitia matembezi ya hisani  kwanzia viwanja vya Nyamagana kupita barabara ya posta pamoja na barabara za Nyerere na Kenyatta. Ambapo zoezi hili ni endelevu na linakusudiwa kutoa elimu katika maeneo mbali mbali ya mkoa wa Mwanza kupitia makundi maalum pamoja pamoja na hospitali na vituo vya afya.

Naye Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiwakilishwa na Katibu wa First Community Bi. Florah Magabe amesema, Mhe Mabula anatambua kundi hili maalum la wahanga wa Seli Mundu/Siko Seli hivyo wameishauri  serikali kupitia Bunge la bajeti na imekubali kupitia wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na walemavu kuweka mkakati wa kuondoa ugonjwa wa Siko Seli kuwa ni magonjwa ya kurithi kwa kupitisha bajeti ilitakayo wezesha hospital yaTaifa Mhimbili kuwa na kitengo maalum cha uwekaji wa ute wa mifupa kwa wagonjwa wa Siko seli ifikapo 2019/2020.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: