Meneja wa mkoa wa Shirika la Taifa la hifadhi ya jamii (NSSF) Shaaban Mpendu (aliyeshika kipaza sauti pichani) amesema moja ya changamoto inayofanya shirika hilo kuchelewesha kutoa mikopo kwa wingi kwa wachimbaji wadogo wadogo ni matumizi ya teknolojia duni za uchimbaji, ambayo huchukua muda mrefu hadi kuanza kurejesha mikopo.

Ameyasema hayo jana mbele ya Naibu waziri wa Madini Stanslaus Nyongo alipotembelea Banda la Maonyesho na mfuko huo katika uwanja wa Kalangalala mjini Geita.

Mpendu alikuwa akifafanua juu ya shughuli zinazofanywa na NSSF ikiwemo utoaji mikopo kwa wachimbaji wadogo wadogo wa Dhahabu. .

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukitoa mikopo kwa wachimbaji wadogo kwa nia ya kuboresha uchimbaji wao lakini tatizo kubwa ni uchelelweshaji wa urejeshaji mikopo ambayo husababishwa na matumizi ya teknolojia duni ya uchimbaji wanayotumia,”alisema.

Aliongeza kuwa NSSF hutoa huduma kwa sekta binafsi, zisizo rasmi ili kuhakikisha kuwa wateja wao wanapata huduma kwa urahisi na kwa ukaribu.

Alisema kufuatia sheria mpya ya mifuko ya Hifadhi ya jamii ambayo inalenga kuandikisha watu wote walio sekta binafsi na zisizo rasmi ili wanufaike na mafao yatolewayo na shirika hilo ikiwemo fao la matibabau bure kwa wanachama na familia zao.

NSSF pia inatoa huduma nyingine ikiwa ni pamoja na huduma za mafao ya aina mbalimbali ikiwa ni Pensheni ya uzeeni,Pensheni ya Ulemavu,Pensheni ya Urithi,mafao ya matibabu,mafao ya uzazi,mafao ya kuumia kazini,msaada wa mazishi pamoja mikopo kwa wajasiriamali.

Maonyesho ya teknolojia ya uchimbaji bora wa dhahabu yalianza tarehe 24 Septemba mwaka na kufunguliwa rasmi na Naibu Waziri wa Madini Stanislaus Nyongo Septemba 26 mwaka huu na yatahitimishwa na Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Septemba 30 Mwaka huu.

Share To:

msumbanews

Post A Comment: