Monday, 10 September 2018

NDG. KALLI AKABIDHIWA RASMI OFISI YA CCM NYAMAGANA


Kaimu katibu wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Mwanza Ndg. Mkondya ambaye alikuwa katibu CCM Nyamagana hivi leo amemkabidhi rasmi Ndg. Salum .A.Kalli ofisi ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana kutokea  Ubungo mkoani Dar Es Salaam.

Ndg. Mkondya akimkabidhi ofisi  Ndg. Kalli amemhakikishia ushirikiano muda wote atakapo kuwa anatekeleza majukumu yake. Amemtakia utumishi mwema wenye uadirifu, weredi na kuzingatia Umoja na mshikamano kwa Chama na jumuiya zake. *Nafarijika kuona toka umefika Nyamagana umeanza kazi kwa kiasi, nimatumaini yangu kasi hii izidi maradufu kujenga na kuimarisha Chama Chetu, usimamizi wa Mali zote na kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashika dola chaguzi zote.* Ndg Mkondya amesema.

Naye Ndg. Kalli amemhakikishia Ndg Mkondya kufuata Katiba, Sera, taratibu na kanuni za Chama Cha Mapinduzi kuongoza Nyamagana pamoja na kusimamia maadhimio yote ya ngazi za juu, kuhakikisha Chama kinashika dola na kurejesha mitaa yote 75 iliyopo upinzani, kulinda mitaa yote iliyopo chini ya CCM katika uchaguzi serikali za Mitaa, kushinda uchaguzi mdogo kata ya Mabatini pamoja na uchaguzi mkuu 2020.

Makabidhiano hayo yamefanyika ofisi za CCM Nyamagana na kuhudhuliwa na secretariat ya wilaya.

Imetolewa na,
Idara ya Siasa  na Uenezi,
Wilaya ya Nyamagana
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: