Tuesday, 18 September 2018

NDG. KALLI AASA WANA CCM NYAMAGANA KUDUMISHA UMOJA NA MSHIKAMANO


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum A. Kalli amemewaasa wana CCM kudumisha Umoja na Mshikamano sanjari na kuondoa tofauti za makundi ya kisiasa tunapo elekea marudio ya uchaguzi mdogo Kata ya Mabatini nafasi ya udiwani.

Ndg. Kalli ametoa rai hiyo alipokuwa anaongea na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Mabatini. Ameelekeza uongozi wa CCM Kata kuweka mpango mkakati kwaajili ya ushindi wa kukomboa mitaa yote iliyopo upinzani na kulinda mitaa mitano inayomilikiwa na CCM tunapoelekeaa uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 pamoja na uchaguzi Mkuu 2020. "Moja ya tunu kuu tunayoweza kutunukia Chama Cha Mapinduzi na Mwenyekiti wetu taifa  Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kama kuhakikisha tunashinda marudio ya uchaguzi Mdogo Kata ya Mabatini pamoja na CCM ishike dola chaguzi zote". Ndg. Kalli amesema

Naye Mwenyekiti Kata ya Mabatini Mhe. Paul Yomoto Mpenzemenya akihairisha kikao hicho amemhakikishia Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya kudumisha umoja na Mshikamano wakati wote wa Chaguzi sanjari na kuisimamia serikali ya Kata katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi 2015-2020.

Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi na washiriki wa kikao hicho Ndg. Alfred Said Shija amempongeza Ndg. kalli kwa kikao cha kazi kilichotoa chachu ya mwelekeo wa falsafa ya CCM Mpya Tanzania Mpya, kwa kudhamiria kuleta Mapinduzi ya ufanisi wa kazi pamoja na kuwafikia wananchi kwa Sera za Chama Cha Mapinduzi.

Kikao hicho kimehudhuliwa na Mabalozi wa nyumba kumi 64, Wenyeviti wa serikali za mitaa pamoja na kamati ya siasa ya Chama Cha Mapinduzi ya Kata ya Mabatini.

Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi Nyamagana
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: