Wednesday, 5 September 2018

Mtu mmoja adakwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji Babati


Jeshi la polisi mkoa wa Manyara linamshikilia mtu mmoja mkazi wa Negamsi mjini Babati Mkoani Manyara aliefahamika kwa majina ya Chadema Horay[25] kwa  tuhuma za Mauaji.

Tukio hilo limetokea wakati wa ugomvi wa marehemu na mkewe baada ya mke kujenga nyumba bila ya kumshirikisha mume wake ndipo mtuhumiwa alipochukua tofali na kumshambulia marehemu aliyekuwa anabomoa nyumba yenye mgogoro.

Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga amesema kuwa mauaji hayo yametokea Agosti 4.2018 saa nane mchana na kumtaja marehemu kwa jina la Shadrack Sangu dereva boda boda mkazi wa Negamsii kata ya Bagara mjini Babati.

Mwili  wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya mji wa Babati  Mrara kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: