Sunday, 30 September 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA WAKISHIRIKIANA NA TAASIS YA SOS WAKABIDHI MADAWATI 100 SHULE YA MSINGI SHIGUNGA


Mhe Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana amekabidhi madawati 100 msaada uliotolewa na wadau wa maendeleo taasis ya SOS katika Kata ya Mhandu Shule ya Msingi Shigunga iliyokuwa na uhaba wa madawati 87. Msaada huo umewezesha wanafunzi wote 1257 kukaa kwenye madawati. 

Leo kupitia wadau wa maendeleo SOS tumeleta Madawati 100 nami kupitia mfuko wa Jimbo nitawapatia  shillingi 2,000,000 kwaajili ya ununuzi wa 'photocopy machine' Mhe Mabula amesema.

Hafla hiyo imefanyika katika ziara maalum ya Mbunge Jimbo la Nyamagana katika taasis ya SOS ambapo aliambatana na Uongozi wa taasis ya SOS, Mhe . Sima C. Sima Diwani mwenyeji, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata na matawi, mtendaji wa Serikali na wa mitaa Kata ya Mhandu.

Imetolewa na 
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿

Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: