Thursday, 13 September 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA AMNADI NDG. JAMAL MGOMBEA UDIWANI KATA YA KIZOTA

Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula ameungana na wakazi wa Dodoma kumnadi mgombe udiwani Kata ya Kizota kwa tiketi ya CCM.

Akimnadi Ndg. Jamal Mhe. Mabula amewasihi wana Dodoma kufanya maamuzi sahihi ya kumunga mkono na kumchagua mgombea udiwani kwa tiketi ya CCM. Kwakuwa Dodoma ni makao makuu ya nchi inahitaji kiongozi mwenye uwezo wa kuongoza, msomi, mpenda watu atakayeweza kuisimamia serikali kwa mstakabali wa maendeleo ya Kizota. Jamal ni mgombea mwenye haiba ya uongozi atakayeweza kwenda na kasi ya utendaji wa Serikali ya awamu ya tano yenye falsafa ya Hapa kazi tu chini ya jemedari Dkt John Pombe Magufuli. 


Kampeni hizo zimehudhuliwa na Mbunge mwenyeji Mhe Anthony Mavunde naibu waziri Ofisi ya Rais Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu pamoja na viongozi mbali wa Chama Cha Mapinduzi.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: