Friday, 14 September 2018

MBUNGE JIMBO LA NYAMAGANA AFADHIRI JEZI ZA WAAMUZI LIGI DARAJA LA NNE


Mhe. Stanislaus Mabula Mbunge Jimbo la Nyamagana amekabidhi Jezi na Vitini vya Uwamuzi vyenye thamani ya shilingi 500,000 kwaajili ya waamuzi wanaoshiriki kuendesha  michuano ya kombe la ligi daraja la nne wilayani Nyamagana chini ya usimamizi wa NDFA"Nyamagana District Football Association" kwa mwaka 2018.

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Jimbo la Nyamagana, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Ndg. Ahmed Misanga amesema Jezi na vitini hivyo vya  uwamuzi ni mwendelezo wa ahadi ya Mhe. Mabula kufadhiri kikamilifu ligi daraja la nne wilayani humu ikiwa ni ahadi moja wapo aliyoitoa wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya michezo Karibuni. "Mhe Mabula anawathamini sanaaaa wana michezo, awali alitoa Jezi kwa vikosi 9, Mipira 5 zenye thaamani ya shilingi 4,200,000 na ataendelea kujidhatiti kudhamini michuano hii kwa miaka mitatu 2018-2020 mfululizo." Ndg Misanga amesema.

Kwaniaba ya NDFA Nyamagana District Football Association Ndg. Domicianus Valenco ampongeza Mhe Stanislaus Mabula kuwa mfadhiri mkuu kwa kufadhiri vifaa vyote vya michezo kwa vikosi tisa  vishiriki pamoja na waamuzi wanaoendesha michuano ya ligi daraja la nne."Nachukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Mhe. Mabula kuwa mdhamini mkuu, ametutoa kimasomaso "NDFA" maana kwa mwaka huu hatukuwa na mdhamini yeyote" Amesema

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: