Wednesday, 5 September 2018

KATIBU WA CCM NYAMAGANA AKUTANA NA WAWEKEZAJI


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum A Kalli akiwa na sekretariet ya wilaya amekutana na wawekezaji 42 wa Mali za Chama wilaya kwa Majengo ya barabara ya Nyerere A na B pamoja na soko kuu.

Ndg Kalli ametumia wasahaa huo kujitambulisha kwa wawekezaji hao pamoja na kuwapongeza wote wanaolipa kwa wakati, ikiwa ni kikao chake cha kwanza na wawekezaji hao baada ya kuhamia wilaya ya Nyamagana akitokea Ubungo. Ndg Kalli amefafanua taratibu  za malipo ya pango kupitia TEHAMA ambao ni mfumo mpya na imara na madhubuti unaotumia malipo kwanjia ya mtandao na mihamara pamoja na Bank kupitia numba maalum ya kila mwekezaji.

Akijibu hoja mbali mbali za wawekezaji hao dhidi ya mfumo wa malipo kwanjia ya mihamara na Bank Ndg. Kalli amefafanua kuwa, kila mpangaji atakabidhiwa namba yake binafsi yenye taarifa zake sahihi za uwekezaji, eneo na kiasi cha malipo anayopaswa kulipa isiyoingiliana na taarifa za mpangaji  mwingine na kuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu zote za malipo ambayo yataingia katika account ya pamoja ya CCM. Njia hiyo itawezesha malipo kutekelezeka wakati wowote bila adha wala makato. Ndg Kalli amehitimisha kwa kuahidi ushirikiano wa kibiashara ikiwa ni pamoja kufanya ukarabati wa baadhi ya maeneo ili kuboresha huduma za CCM kwa Wateja wake.

Naye Mhasibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Mary ambaye pia ni katibu UWT wilaya amewahasa wawekezaji kufikisha ofisini kwa wakati  ankla za malipo kwaajili ya kuweka kumbukumbu, pia ametoa tahadhari yakuondoa mkanganyiko wa malipo kwa wawekezaji wanaolipa bank kufanya malipo kupitia majina ya biashara au yaliyoorodheshwa kwenye mkataba kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Akiongea kwa niaba ya wawekezaji wengine Ndg. Privatus ameusifu mfumo mpya wa malipo ya CCM unaowezesha malipo wakati wowote na kulipia fedha kila mwezi ambayo ni rahisi kwa mpangaji yeyote kuufuata.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: