Friday, 7 September 2018

KATIBU KALLI AWAFUNDA WATENDAJI UMOJA WA VIJANA NYAMAGANA


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum A Kalli amewafunda makatibu wa Umoja wa Vijana pamoja na  makatibu Chipukizi na Hamasa kutokea kata zote 18 za wilaya ya Nyamagana.

Huu umekuwa ni mwendelezo wa vikao vya kikazi kwa Ndg. Kalli kuwafikia watendaji Wote wa Chama Cha Mapinduzi na jumuiya zake zote, wawekezaji wa mali za Chama, dhima kuu ikiwa ni kujenga na kuimarisha Chama Cha Mapinduzi. Ndg Kalli akiwa na makatibu Chipukizi na Hamasa pamoja makatibu Umoja wa Vijana wa kata zote 18,  ametumia adhara hiyo kuwasihi kutumia nafasi zao kukisemea Chama Cha Mapinduzi pamoja na utekelezaji wake wa Ilani ya uchaguzi 2015-2020,  kutetetea maslahi ya wanyonge na kusimamia haki ambayo ndio msingi  wa falsafa ya CCM Mpya na Tanzania Mpya.

Ndg. Kalli  amewataka watendaji hao kuwa chachu katika Umoja huo sanjari na kuvunja makundi na kutoyandekeza kwani hayana afya kwa mstakabali wa Chama Madhubuti. Amewahasa Vijana kusimamia kweli, haki, kuimarisha upendo na mshikamano baina yao kwakuakisi sera za CCM pamoja na miongozo ya katiba pamoja na kanuni mpya CCM ya fedha ya 2018. Amesema ni busara watendaji Wote kuzingatia kanuni na taratibu mbali mbali katika uendeshaji wa shughuli za chama,  kuweka mikakati inayojipambanua katika misingi ya siasa safi na uchumi imara, kwa kuimarisha uchumi wa jumuiya kupitia ubunifu wa  vyanzo vipya vya mapato, na kuhakikisha Umoja wa Vijana unasimamia halmashauri iweze kutoa 5% ya mapato yake kupitia mfuko wa maendeleo ya Vijana na wanawake ya mapato ya 10% ya halmashauri.

Ndg Kalli amehitimisha kwa kuhasa upendo, umoja na mshikamano kama nguvu dhabiti tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 pamoja na uchaguzi mkuu 2020. Kwa watendaji wote kuandaa mipango mikakati ya kisiasa  ili kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi kinashinda mitaa 175 yote ya halmashauri ya jiji la Mwanza na kukomboa mitaa yote 75 iliyopo upinzani, hivyo maandalizi yote ya kimkakati yaanze Sasa. *Sitarithi adui ya mtu, na wala sitatengeneza adui bali nimekuja hapa kuhakikisha CCM inashika dola serikali za Mitaa na serikali kuu 2020, naomembeni ushirikiano* Ndg. Kalli amesema

Akifungua kikao hicho kaimu katibu wa Umoja wa Vijana Nyamagana ambaye ndio katibu wa Kikao hicho Ndg. Barnabus Mpuya akimkalibisha katibu wilaya Ndg Kalli amesema umoja wa Vijana Nyamagana ni miongoni mwa jumuiya imara na iko tayari kushirilikiana na Chama katika nyanja mbali kwaajii ya mstakabali wa ujenzi na uimarishaji wa Jumuiya na Chama Cha Mapinduzi. Kwa kuenzi falsafa ya Kazi tu Umoja huo umeridhia kuwa na vikao vya kikazi mara mbili kila mwezi tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019.

Akiongea kwa niaba ya wajumbe katibu wa Chipukizi na Hamasa Ndg. Joseph Allianus amempongeza Ndg Kalli kwa Kazi yake ya utendaji aliyoanza anayo imetia hamasa na kuleta mshikamano baina ya watendaji, hivyo amemwahidi kuzidi kuimarisha Umoja na mshikamano na kuzidi kukisemea Chama Cha Mapinduzi kwa ngazi yaWilaya pamoja na Kata kuhakikisha CCM inazidi kuimarika na kuongeza idadi ya wanachama wapya. 

Imetolewa na
Idara ya Siasa na Uenezi
Chama Cha Mapinduzi Nyamagana
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: