Katibu wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana Ndg. Salum A Kalli ameanza kazi kwa kasi wilayani humu, kwa kukutana na watendaji wa kata zote 18.

Ndg. Kalli akiwa ndio mwenyekiti wa kikao chake cha kwanza baada ya kuhamia Nyamagana akitokea Ubungo, amekutana na watendaji wote wa Kata 18  wa wilaya ambapo ametoa mwelekeo wa falisafa ya CCM mpya Tanzania Mpya. Ameelekeza Chama kwa ngazi za Kata na Matawi kufuata na kuzingatia kanuni ya fedha ya CCM ya mwaka 2018, ikiwa ni  mapato yote kufuata mfumo wa TEHAMA unaoweka mapato yote ya Chama  katika account ya pamoja kwanzia ngazi ya Tawi, Kata, wilaya, mkoa hadi taifa. Hivyo Chama Cha Mapinduzi Nyamagana na jumuiya zake zote Umoja wa Wanawake, Vijana na Wazazi  inapaswa kufungua akaunti kupitia Bank ya CRDB na endapo itahiji kutumia fedha iwasilishe maombi ya matumizi kila tarehe 18 ya mwezi. Mfumo utakaowezesha mapato kwa kila kwa 10% ya mapato kwenda Kata, 25% wilayani, 15% Mkoani na 50% kubaki eneo la mradi.

Akijibu hoja na mapendekezo ya watendaji Ndg. Kalli. amehasa uzalendo, ubunifu, uibuaji wa miradi mipya, uwaminifu na dhamira njema kwa watendaji wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuwa na Chama madhubuti na kimbilio la wanyonge na Chama chenye mvuto kwa wananchi wote, dhana itakayo wezesha uimarishaji wa Chama na jumuiya zake. Pia amelekeza uzingatiwaji wa vikao vya kikanuni kwa kamati za siasa na halmashauri za kata na matawi  pamoja na watendaji hao kuwa na kikao cha kikazi kila wiki utaratibu utakao shuka ngazi ya Kata na matawi. Ndg Kalli amefafanua CCM inajengwa na Vikao na vikao vya kazi vitasaidi umoja na mshikamano tunapoelekea uchaguzi wa serikali za mitaa 2019 na serikali kuu 2020 pamoja na uimarishaji wa Chama.

Ndg Kalli amehitimisha kwa kusisitiza ufuataji wa protocal wakati wa mikutano, utaratibu na kanuni katika uendeshaji wa Chama sanjari na uwekaji mikakati madhubuti ya kushika dola pamoja na kuisimamia serikali kwa ngazi zote. Amewaasa watendaji wa Kata kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi Kata  kuhakikisha Wawakilishi wa wananchi ngazi ya Kata na mitaa yote kuwa na vikao vya uwasilishaji wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi 2015-2020 pamoja na usomaji wa taarifa za mapato na matumizi kwa wananchi.

Wakiongea kwa nyakati tofauti Mhasibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Mary ambaye pia ni katibu UWT wilaya amesisitiza utaratibu wa uwasilishaji ankla za malipo kila mwezi pamoja na utaratibu wa mapato na matumizi kwa Chama pamoja na jumuiya zake kupitia TEHAMA. Naye katibu wa Wazazi Bi Zamda Kamgisha ameasa watendaji ngazi ya kata kujali na kuthamini jumuiya zote katika mstakabali wa ujenzi wa Chama Cha Mapinduzi.

Kikao  kimehudhuliwa seketariet ya  Wilaya ya Nyamagana pamoja na watendaji wa kata zote 
18 chini ya katibu wa wilaya Nyamagana ambaye ni mwenyekiti wa kikao.

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Nyamagana🇹🇿





Share To:

msumbanews

Post A Comment: