Diwani wa kata ya Olasiti  Katika Jiji la Arusha kupitia (Chadema), Ndg.Alex Marti ameamua  kuandika  barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na chama chama Mapinduzi CCM kwa maelezo kwamba anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Alex Marti  ni diwani wa nane katika Jiji la Arusha  kujiuzulu kwa kipindi hiki kwa kufurahishwa na utendaji kazi wa  Rais John Pombe  Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, amethibitisha leo ( September 02, 2018 ) kupata taarifa za kujiuzulu kwa diwani huyo Ndg .Alex Marti

Share To:

msumbanews

Post A Comment: