Thursday, 27 September 2018

DC Ngubiagai atoa agizo zito kwa watumishi wa Halmashauri


Na.Ahmad Mmow,Kilwa.
MKUU wa wilaya ya Kilwa, Mkoa wa Lindi, Christopher Ngubiagai ameita Halmashauri ya Wilaya hiyo iwalipe fidia wananchi waliotoa maeneo yao kwa halmashauri hiyo.

Ngubiagai alitoa agizo hilo kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashsuri hiyo kilichofanyika katika mamlaka ya mji mdogo wa Kilwa Masoko.

Ameitaka halmashauri hiyo ihakikishe katika fedha zinazokusanywa zinatumika kuwalipa wananchi fidia ya maeneo yao ambayo yamechukuliwa na halmashauri kwani amechoshwa kusikia kuhusu madai hayo.

Alisema wananchi wengi wanamlalamikia yeye na amejitahidi sana kufuatilia ili wananchi hao walipwe fedha hizo ambazo ni haki yao hata hivyo bado madai mengi hayajashugulikiwa.

" Mnauza viwanja vya wananchi lakini hamtaki kuwalipa wazee wanatembea na karatasi wanataka kuanguka barabarani kuja kulalamika ofisini kwangu fedha zikiingia muanze kuwalipa,"alisisitiza Ngubiagai.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: