Mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma, Bi. Sophia Kizigo amepiga marufuku tabia ya baadhi ya viongozi kuteketeza mashamba na mazao ya wakulima waliolima kwenye Mabonde na Hifadhi za Taifa katika wilaya hiyo na kuwataka kufanya doria za mara kwa mara na kutoa elimu kwa wakulima hao kuhusu athari za kulima kwenye hifadhi hizo badala ya kusubiria mazao yao yakomae na kufikia hatua ya kuvunwa.

Mkuu huyo wa wilaya ya Namtumbo,Bi.Sophia Kizigo amepiga marufuku hiyo katika kikao chake cha kwanza kwenye Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo tangu ateuliwe hivi karibuni na rais na kudai tabia ya kuwavizia wakulima walime na mazao yao kukomaa ndipo yateketezwe haukubaliki.

Hata hivyo baadhi ya madiwani wa halmashauri ya Namtumbo wamedai,utekelezaji wa maagizo mbalimbali yalikuwa magumu kutekelezeka kutokana na mifarakano mikubwa waliyokua nayo kati yao
Share To:

msumbanews

Post A Comment: