Diwani wa kata ya Oldnyosambu  katika Halmashauri ya Arusha  kupitia (Chadema), Ndg. Raymond  ameandika barua ya kujiuzulu udiwani na kujiunga na chama chama Mapinduzi CCM kwa maelezo kwamba amefurahishwa na utendaji kazi na anamuunga mkono Rais John Magufuli.

Raymond ni diwani wa tatu katika Halmashauri ya Arusha kujiuzulu kwa kipindi hiki na kujiunga na CCM kwa kumuunga mkono Rais Magufuli.

Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Dkt. Wilson Mahera amethibitisha leo ( 07 September 2018 ) kupata taarifa za kujiuzulu kwa diwani huyo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: