MBUNGE WA KIGOMA MJINI (ACT WAZALENDO), ZITTO KABWE.

MBUNGE wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe, amelalamikia Jeshi la Polisi kutokana na kuendelea kushikilia simu yake kwa miezi tisa sasa.

Novemba 7, mwaka jana, Jeshi la Polisi lilichukua simu ya mbunge huyo kwa madai ya uchunguzi kuhusu tuhuma kwa mujibu wa sheria ya takwimu na sheria ya makosa ya mtandao.

“Walisema watahitaji simu hiyo kwa siku mbili tu. Nilikwenda Kituo cha Polisi Kamata siku  ya tatu nikaelezwa kuwa bado wanaendelea na uchunguzi.

Hata niliporudi tena siku nyingine polisi walisema bado wanahitaji simu yangu”, alisema Zitto jana alipozungumza na Nipashe kuhusu kushikiliwa kwa simu yake kwa muda wote huo.

Nipashe ilimtafuta Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, ili kujua hatima ya simu hizo lakini  simu yake iliita bila kupokewa.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: