Friday, 3 August 2018

Zawadi ya Miss Lake Zone yapingwa kwa kutokuwa na hadhi


Na James Timber, Mwanza
Kampuni ya The Look yenye dhamana ya kusimamia mashindano ya Miss Tanzania   imesikitishwa na zawadi waliyoiandaa waandaaji wa mashindano ya Miss Lake Zone ambao ni Jembe ni Jembe Group ya jijini Mwanza kuwa haiendani na hadhi ya kupewa mshindi bali watafute zawadi nyingine.

Hayo yamejiri baada ya hapo jana Waandaaji wa Mashindano ya Miss Lake Zone kutangaza zawadi mbalimbali kwa washindi na washiriki ikiwemo pesa taslimu na gari kwa mshindi wa kwanza, ambapo ilizua mijadala kibao kwenye mitandao ya kijamii kuwa inawezekana likawa limetumika.

Hata hivyo Mashindano hayo yanatarajia kufanyika Agosti 4, Mwaka huu katika Viwanja vya Rock City Mall jijini hapa kutokana na taarifa yao kwa Vyombo vya Habari Agosti 2, Mwaka huu, ambapo warembo 15 kutoka Mikoa ya Geita, Mara na Mwanza watashiriki.
Previous Post
Next Post

post written by:

0 comments: