Julie Genter na mwenza wake

Waziri wa masuala ya wanawake huko New Zealand Ameendesha baiskeli hadi hospitali kujifungua mtoto wake wa kwanza.


Julie Genter kutoka chama cha kijani, Green party, amesema kuwa ameenda kwa baiskeli kwakua hakukua na nafasi ya kutosha ndani ya gari, alipiga picha na mweza wake wakiwa katika safari hiyo ya baiskeli na kuiweka katika akaunti yake ya Instagram.

Mwezi juni mbunge Jacinda Ardern alikua wa pili kujifunglia katika sehemu ya kazi, wote yeye na Bi Genter walikua wakihudhuria Clinic pamoja katika hospitali ya umma huko mji Auckland.

Bi Genter 38, anajulikana sana pia kama mdau mkubwa katika kuendesha baiskeli, aliandika katika mtandao wake wa Instagram, ''mtuombee Baraka, mimi na mwenzangu tumepanda kwenye baiskeli kwasababu hakukua na nafasi kwenye gari kutokana na wasindikizaji kukaa kote.

Waziri huyo atachukua miezi mitatu ya likizo ya uzazi, ataungana na baadhi ya wanasiasa waliopata watoto wakati wanatumikia nafasi za kisiasa.Julie Genter

Mbunge wa kwanza kupata mtoto akitumikia bunge la New Zealand, ilikua mwaka 1970, huku mwingine akinyonyesha kwa mara ya kwanza katika eneo la kazi mwaka 1983.

Nao Austalia walibadilisha kanuni mwaka 2016 kuruhusu watunga sheria kuweka sheria ya kunyonyesha katika eneo maalumu ndani ya bunge.

Katika miaka ya hivi karibuni, Sweden, Italia na Bunge la Ulaya wamegusa ulimwengu kwa upigaji kura wakiwa wamebeba watoto.
Chanzo-BBC
Share To:

Anonymous

Post A Comment: