Leo nieleze kidogo sababu ya rai ya Mwenyekiti wa CCM na  Rais wa Tanzania Ndg John Pombe Joseph Magufuli aliyoitamka wiki chache zilizopita ya kuwa "CCM itatawala milele". Ambayo imeonekana kupigiwa kelele na Wapinzani.

- Udhaifu wa upinzani

Ifahamike kuwa CCM kuendelea kuongoza inategemea udhaifu wa vyama vya upinzani hapa Tanzania. Udhaifu huu unatokana na aina ya Vyama vilivyopo, Dira ya Vyama hivi, Itikadi, Sera, ajenda na zaidi wamechagua kuunga mkono kundi gani katika jamii ya watanzania.

- Chama ni Watu

Ijulikane kuwa hakuna Chama cha siasa Duniani kinachoweza kupiga hatua za uhakika na kuwa na uungwaji mkono wa kudumu ( permanent voters) kama Chama hakijajinasibisha na jamii fulani ya watu. Mfano leo hii vyama vikubwa Duniani huwa vimegawanyika katika makundi kadhaa, yaani vyama vya makabwela, vyama vya Wakwasi, ama vyama vya wafanyakazi, Kihafidhina n.k.

- Chama ni Icon (utambulisho)

Chama cha siasa madhubuti ni lazima kiwe na utambulisho (Icon) yaani kikitamkwa kuna taswira (Image) inakujia akilini ya kukutambulisha aina ya Jamii inayowatetea, na kuwa na jamii ni lazima Chama kiwe na Itikadi, Sera, na ajenda mahususi na hivyo ndio huvutia tabaka fulani la watu katika Jamii, na hiyo huwa haijengwi katika usiku mmoja huwa ni kuanzia vizazi vitatu mpaka vizazi vinne na ikumbukwe tu kuwa kizazi kimoja ni miaka ishiririni na mitano, hivyo kuweza kujenga Chama cha Siasa Chenye wapiga kura wa kudumu ni ujenzi usiopungua miaka 50 - 75 mpaka 100.

- Chama si wafuasi binafsi

Kutokana na ugumu wa ujenzi wa Chama Cha Siasa, vyama vingi vya upinzani vimeshindwa kujijenga Kiitikadi, Kisera, wala kuwa na ajenda muhususi hivyo kukosa wapiga kura wa kudumu hivyo muda wote kubakia na wapiga kuwa wa hasira wenye matakwa binafsi,  mihemko, na wagombea wao kuwa na wafuasi binafsi (pocket voters) kama ilivyokuwa 2015, ambao wengi wao baada ya muda mfupi, hupata akili zao kamili na kuanza kurudi CCM kama ilivyo sasa.

- Chama ni ujenzi wa Misingi

Ujenzi wa CCM mpya leo ni kazi iyoihakikishia CCM ushindi kwa zaidi ya vizazi viwili kuanzia sasa, maana hakuna mtanzania anayependa Rushwa, uzembe kazini, kuminywa haki, n.k ambapo vyote hivi vinapigwa vita na CCM mpya na si Chama kingine Chochote hapa Tanzania. Kwa hali hiyo tu tayari CCM inatengeneza wapiga kura wa kudumu 80% kwa miaka zaidi ya 50.

- Chama ni dhamira ya dhati

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema juu ya udhaifu wa vyama hivi hata shabaha ya uanzishwaji wake  na dhamira za waanzilishi. Mwaka 1995 wakati huo Mwenyekiti wa CHADEMA akiwa Mzee Mtei,  Mwalimu nyerere aliwahi kuwaambia Watanzania kuwa, "Vyama hivi vya upinzani ni vyama vya ruzuku, vingi huibuka kipindi cha uchaguzi na kupotea kabisa baada ya uchaguzi", yaani visivyo na Itikadi, Sera, wala Dira na kufanya visiwe mbadala hivyo kuipa CCM muda mrefu wa kuendelea kuongoza.

- Chama ni ukubalifu

Kwa sasa CCM imeweza kujinasibisha na kundi kubwa la watu wenye vipato vya chini na kati zaidi hata Mwenyekiti wake Ndg. John Joseph Magufuli amejitambulisha hadharani kuwa yeye ni Rais wa wanyonge, hivyo tayari CCM imetengeneza wapiga kura wa kudumu. Tofauti kabisa na Vyama vingine ambavyo sasa hawaelewi wasimame na watu wa aina gani ili kutengeneza wapiga wa kudumu.

- Chama ni muda

Rai yangu, Vyama vya upinzani visiwe na haraka ya kuongoza, vianze kwanza kujijenga kabla ya kuomba kuaminiwa ila viendelee kushiriki katika Chaguzi ili viimarike zaidi.

Na mwandishi wetu.
Said Said Nguya
Saidnguya@gmail.com
Share To:

msumbanews

Post A Comment: