Mbunge wa Chalinze, MH.RIDHIWAN KIKWETE ameishukuru serikali kwa kulipatia Halmashauri ya Chalinze shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya katika maeneo ya Kibindu,Mkange na Lugoba katika kusogeza huduma ya afya kwa wananchi.

Ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa vifaa vya ofisi kutoka Taasisi ya TANZANIA HEALTH PROMOTION SUPPORT, Ambapo amesema fedha hizo zimetolewa katika kutekeleza mpango wa kujenga vituo vya afya katika halmashauri ya Chalinze na kwa sasa kituo cha afya Kibindu kimepatiwa shilingi milioni 420 na kituo cha afya Mkange kimepata katika hatua za mwisho kukamilika na milioni 700 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Lugoba.

MH. KIKWETE amesema mpaka sasa serikali imetoa madaktari 47 kwa halmashauri ya wilaya ya Chalinze katika kupunguza tatizo la watoa huduma ya afya na Katika Hospitali ya wilaya Msoga watapata madaktari 10 ili kuimarisha huduma.

MH.KIKWETE amesema msaada huo wa serikali ni msaada mkubwa kwa wananchi wa halmashauri ya Chalinze katika suala zima la kupata huduma za afya na kielelezo kinachoonyesha jinsi gani serikali imekuwa bega kwa began na wananchi katika kuhakikisha wananchi hawatembei umbali mrefu kupata huduma hiyo muhimu.

Naye mwakilishi wa THPS, BW.SISTY MOSHI amesema taasisi yao kupitia usaidizi wa Serikali ya Marekani imekuwa inasaidiana na serikali katika utoaji wa huduma ya afya.

Ambapo kwa sasa imekuwa ikijihusisha katika utoaji wa huduma katika mikoa ya Kigoma, Pwani na Zanzibar na ikijielekeza Zaidi katika utoaji wa huduma ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa UKIMWI katika utoaji wa huduma na tiba.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: