Mkuu wa Mkoa Ally Hapi akisalimia na wazee wa Wilaya ya Kilolo alipofanya ziara yake ya kujitambulisha wilayani humo.

MKuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah akisoma taarifa Wilaya kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Ally Hapi, alipofanya ziara wilayani hapo kwa ajili ya kujitambulisha. (Picha zote na Datus Mahendeka).



NA Datus Mahendeka (OuT)

MKUU mpya wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi, amesema atahakiki na ufanisi wa utendaji wa kila mtumishi au mkuu wa Idara ndani ya Wilaya ya Kilolo.
Akizungumza na watumishi na wakuu wa Idara mbalimbali wa Wilaya ya Kilolo katika ziara yake ya kwanza ya utambulisho ambapo alisema, lengo kubwa ni kuijenga Iringa mpya.

“Kwangu kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, na ile dhana na kupeana taarifa kwa makaratasi tutaona uhalisia wake pindi tukija site (eneo la mradi), ili taarifa hizo ziwe sambamba na kinachonekana”alisema

Alifafanua kuwa, amepanga ratiba ya siku 18 zenye lengo la kutembelea kila Tarafa, kukagua, kufungua, kufuatilia miradi ya maendeleo ndani ya Wilaya zote za Iringa.Alisema Mkurugenzi ni vyema kuwa na taarifa za kila wiki za watendaji wake ikiwemo wamefanya nini au wiki ijayo wanatarajia kufanya kitu gani ili mishahara na posho walipwe kwa haki.

Alisema ni vyema watendaji hao waaachana na utendaji wa mazoea, kutengeneza chuki baina ya Serikali na Wananchi kutokana na kutoshughulikia matatizo ya watu.Aliongeza kuwa uzoefu unaonyesha kuna baadhi ya watendaji hawajatatua mgogoro wa aina yoyote ndani ya sehemu yake, hivyo ni lazima wawe mfano kwa kuatua na kuwa ripoti ya wiki ya utendaji wao wa kazi.

Aidha, alisema ni vyema watendaji hao na wakuu wa vitengo kwenda kwa Wananchi badala ya kukaa ofisi, ili kujiridhisha na taarifa zenye kusifia kuwa hali ni nzuri.Aliongeza kuwa wakuu wa Idara wana vitendea kazi mbalimbali ikiwemo magari, hivyo ni lazima wazunguke kwa Wananchi kwa lengo la kuwasikiliza na kutatua kero zao.

Pia aliwataka kuwa waadilifu, kutojihusisha na vitendo vya rushwa kutoka kwa Wananchi kwani wanalipwa mshahara kutoka kwa Wananchi hao, pamoja na kutunza siri mbalimbali za ofisi na taarifa za vikao.liongeza kuwa ushirikiano baina ya watendaji na wakuu wa Idara na watumishi wengine itakuwa nguzo ya maendeleo na kutimiza lengo la kuwa Iringa mpya.

Hata hivyo aliwapongeza kwa kazi nzuri wanayoifanya kwenye Nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo elimu na kilimo.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: